Thursday 25th, April 2024
@Ukumbi wa Halmashauri
Katibu Mkuu wa Tume ya Huduma kwa Walimu Mwl. Winfrida G. Rutaindurwa atafanya ziara ya kikazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda akiwa na lengo kuu la kuzungumza na Walimu na Viongozi wa Idara za Elimu Msingi na Sekondari.
Katika mazungumzo hayo, katibu huyo atapata fursa ya kusikiliza Changamoto mbalimbali toka kwa Washiriki ikiwa ni pamoja na kutoa ufafanuzi wa Sheria mbalimbali za kiutumishi hasa zile zinazolenga Sekta ya Elimu nchini.
Mazungumzo hayo yatafanyika siku ya Jumanne Tarehe 25/10/2017 katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda kuanzia saa 2.00 asubuhi ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Bunda Ndg. Lydia Bupilipili.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0754821313
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda