Thursday 28th, March 2024
@Kibara, Bunda
Siku ya Ukimwi Duniani inaadhimishwa kila tarehe 1 Desemba kama siku maalumu ya kupanua ufahamu kuhusu maafa yanayoletwa na ugonjwa wa Ukimwi.
Desemba mosi ilichaguliwa kuwa siku ya Ukimwi kutokana na tarehe hiyo kuwa ndiyo siku ambayo virusi cha Ukimwi kilitambulika rasmi mwaka 1981. Toka mwaka 1981 hadi 2007 watu zaidi ya milioni 25 wameshafariki kutokana na Ukimwi. Mwaka 2007 peke yake walifariki milioni 2, kati yao watoto 270,000. Siku hiyo ilichaguliwa rasmi mwaka 1988 wakati wa Mkutano wa Dunia wa Mawaziri wa Afya Kuhusu Mpango wa Kuzuia Ukimwi. Kuanzia hapo siku hiyo imekuwa ikikumbukwa rasmi na serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali, na wanaharakati. Toka mwaka 1988 hadi 2004, Siku ya Ukimwi Duniani ilikuwa ikiratibiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Ukimwi (UNAIDS). Mwaka 2005 UNAIDS ililipa shirika lisilo la kiserikali la Kampeni ya Ukimwi Duniani (the World AIDS Campaign) wajibu wa kuratibu siku hiyo. Kila mwaka siku hiyo hufanyika kwa ujumbe maalumu. Ujumbe wa mwaka 2005 hadi mwaka 2010 ulikuwa, "Zuia Ukimwi: Timiza Ahadi".
Halmashauri ya Wilaya ya Bunda itaadhimishwa siku hii katika Kata ya Kibara ambapo Wananchi na Viongozi mbalimbali wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Bunda Ndg. Lydia Bupilipili watakutana na kutafakari ikiwa ni pamoja na kukumbushana juu ya tatizo hili la VVU/UKIMWI kama njia mojawapo ya kupunguza kasi ya ueneaji wake. Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni "Changia kwenye Mfuko wa Udhamini katika kupambana na UKIMWI wilayani Bunda"
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0754821313
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda