Saturday 20th, April 2024
@Ketare
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda anawatangazia wananchi wote kuwa, Halmashauri inatarajia kuadhimisha sherehe za siku ya wanawake duniani. Maadhimisho hayo yatafanyika katika Kata ya Ketare siku ya tarehe 8/3/2018 kuanzia saa 3:00 asubuhi. Kauli mbiu ya maadhimisho hayo inasema “KUELEKEA UCHUMI WA VIWANDA, TUIMARISHE USAWA WA KIJINSIA NA UWEZESHAJI WANAWAKE VIJIJINI’
Kupitia maadhimisho hayo wanawake watapata fursa ya kuonyesha shughuli mbalimbali za ujasiliamali wanazozifanya.
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo atakuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mhe. Mwl. Lydia Bupilipili.
Wote mnakaribishwa
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0754821313
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda