Friday 29th, March 2024
@Mugeta Ward
Timu ya watu 8 toka Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji (W) na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda inatarajia kufanya ziara katika maeneo yaliyofanyiwa uharibifu wa Mazingira Kata ya Mugeta katika Vijiji vya Kyandege,Tingirima na Mugeta ambavyo vinapakana na Pori la Akiba Grumet ili kujionea hali halisi ya uharibu huo na chanzo chake ili kuchukua hatua stahiki za kukomesha uharibifu huo.
Wakati wa Ziara, timu hiyo itakutana na Viongozi wa jumla ya Vijiji 7 ambavyo ni Kyandege, Tingirima, Mugeta, Mariwanda, Sarakwa, Kihumbu na Hunyari kutoa mrejesho wa ziara husika kwa viongozi hao juu ya hali halisi ya uharibifu wa Mazingira katika Vijiji vilivyotembelewa, aidha Mwenyekiti wa Halmashauri atatoa hundi kwa vijiji hivyo ambayo ni pesa toka Wizara ya Maliasili na Utalii ikiwa ni sehemu ya 25% ya mapato ya uwindaji wa kitalii katika pori la Grumet. Pesa hiyo huwa inatolewa kwa ajili ya kusaidia shughuli za Uhifadhi wa Maliasili na Maendeleo ya Vijiji.
Pamoja na Mkurugenzi Mtendaji na Mwenyekiti wa Halmashauri, timu hiyo pia itakuwa na Kaimu Afisa Ardhi na Maliasili, Afisa Misitu, Afisa Habari wa Halmashauri na Waandishi wa Habari.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0754821313
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda