Elimu ya kujikinga na Corona Yatolewa kwa Wananchi Halmashauri ya Wilaya Bunda
Kutokana na Uwepo wa ugonjwa wa corona nchini Tanzania,Halmashauri ya Wilaya ya Bunda imeanza kutoa elimu kwa Wananchi wake ili kuweza kuchukua tahadhari za kujiepusha na maambukizi dhidi ya virusi vya corona.
Akizungumza katika kipindi Maalum kilichofanyika Mazingira Fm Machi 22,2020. Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya Dkt.Nuru Yunge amesema virusi huwa vina jamii tofauti kwa virusi vya corona ni virusi ambavyo vinasababishwa na homa kali ya mapafu ,hupelekea mtu kushindwa kupumua, ,vidonda kooni na dalili nyingine.Ugonjwa huu unaweza kuepukika pale itakapuchukuliwa tahadhari.
Yunge amewaeleza wananchi kuhakikisha wanafuata maelekezeo yanayotolewa na watalaam wa afya ilikuendelea kujikinga na Ugonjwa huu kwa kunawa mikono kila wakati kwa maji yanayotiririka na sabuni,kuepuka kusalimiana na kwa kushikana mikono,kukumbatiana ,kuepuka kugusa macho,pua na mdomo,kufunika mdomo wakati wa kukohoa kwa kutumia kitambaa kisafi au sehemu ya mkono.‘Wananchi wasiwe na hofu zaidi tuendelee kujikinga”
Aidha Halmashauri ya Wilaya Bunda imetenga eneo maalumu katika kituo cha afya Kisorya, na Ikizu ambapo endapo kutabainika au kuhisiwa mgonjwa mwenye dalili za virusi vya corona atawekwa chini ya uwangalizi kwa siku 14 katika vituo taja.
Mwisho alisisitiza wananchi kuepuka misongamano isiyoyalazima kuchukua tahadhari ni muhimu ili kuepuka na maambuki ya virusi vya corona .alisema dkt Yunge
Mmoja wa wasikilizaji wa kipindi hicho cha Radio Bi. Nyangeta alitoa shukurani kupitia ujumbe mfupi wa meseji kwa kupata elimu kuhusu ugonjwa wa virusi vya corona
Ugonjwa wa virusi vya corona vilianza rasmi china katika Mji wa Wuhan,na kusambaa nchi mbalimbali na kwa Tanzania mgonjwa wa kwanza aligundulika Jijini Arusha mnamo Machi16,2020.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0754335739
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda