Mkuu wa mkoa wa Mara Mhe.Ally Hapi amewataka wazazi kuendelea kuwapeleka watoto Shuleni ili waweze kupata Elimu kwa manufaa ya baadae.
Mhe.Hapi amesema hayo Januari 21,2022 mara baada ya kukabidhiwa vyumba 87 vya madarasa ambavyo fedha zake zimetokana na mpango wa maendeleo ya Ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya Uviko-19.
Mhe. Hapi amesema kuwa kila mzazi ambae mtoto wake anatakiwa kwenda shule ampeleke kwasababu serikali imeendelea kutoa elimu bure na kutengeneza mazingira bora ya kujifunza.
“Serikali haitamvumilia mzazi yeyote ambae hatompeleka mtoto shule,wazazi ni wajibu wenu kupeleka watoto shule"amesisitiza Mhe Hapi
Aidha Mhe.Hapi amesema kuwa Serikali imeendelea kuweka mazingira bora kwa walimu na wanafunzi ili kuongeza ufaulu .
“Serikali inaendelea kulipa madai ya walimu,kupandisha madaraja pamoja kuweka mazingira bora ya kufundisha na kujifunza”Mhe.Ally Hapi
Awali akitoa taarifa ya ujenzi wa madarasa hayo mwalimu Frolian Phares Kamugisha kutoka Shule ya Sekondari Makongoro amesema kuwa madarasa mapya yamesaidia kupunguza msongamano kwa wanafunzi darasani pamoja na kuweka mazingira rafiki ya kufundisha na kujifunza.
Aidha mwalimu Kamugisha ametoa shukrani kwa Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kwakuwapatia kiasi cha sjhilingi 80,000,000 kwaajili ya ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa na ofisi mbili
‘’Tunamshukuru Mhe.Rais kwakutupatia mgao wa fedha hizo ambapo leo hii mazingira mazuri katika shule imekua faraja kwa walimu pamoja na wanafunzi’’amesema Mwal.Kamugisha
Mwisho Mkuu wa Mkoa amefanya Mkutano wa hadhara na kuzungumza na wananchi wa Kata ya Nyamuswa na Kata jirani sambamba na kusikiliza kero za wananchi.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0754335739
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda