Kwa mara ya kwanza ndani ya kipindi cha miaka mitano (5) Halmashauri ya Wilaya ya Bunda imevunja rekodi ya makusanyo ya mapato yake ya ndani baada ya kukusanya jumla ya shilingi 1,236,797,332/= kiwango ambacho hakijawahi kufikiwa ndani ya kipindi hicho. Kiasi hiki kimerekodiwa kwa mwaka wa fedha wa 2021/2022 kama kilivyothibitishwa na Kaimu Mweka Hazina wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Bw. Romanus Komba.
Hata hivyo, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Mhe. Bashungwa hapo jana tarehe 02/08/2022, Halmashauri ya Wilaya ya Bunda ilionekana kukusanya mapato ya ndani kwa asilimia 70 tu. Hii ni kutokana na ukweli kuwa maoteo /makisio ya makusanyo kwa mwaka huo wa fedha yalikuwa juu zaidi kwa vipindi vyote vitano (5), yaani 2017/2018 hadi 2021/2022.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0754335739
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda