Mwenge wa uhuru.2024 umewasili mkoani Mara na kupokelewa na katibu Tawala wa Mkoa wa Mara, Ndugu Gerald Kusaya siku ya tarehe 26/7/2024 katika viwanja vya shule ya msingi Robanda, wilayani Serengeti.
Ndugu Kusaya alipokea mwenge wa uhuru kutokea mkoani Arusha kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi.
“Mwenge wa uhuru katika mkoa wa Mara utakimbizwa katika Wilaya sita na Halmashauri Tisa, ambapo, utakagua, kutembelea, kuzindua na kuweka mawe ya msingi katika miradi 72 ya maendeleo iliyopo Mkoani Mara, katika wilaya na Halmashauri zote Tisa.” Alisema Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara.
Kauli mbiu “TUNZA MAZINGIRA NA SHIRIKI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KWA MAENDELEO YA TAIFA ENDELEVU.”
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0754335739
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda