Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, Bi. Changwa M. Mkwazu amefanya kikao kifupi na Wadau wa Maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya, Wadau hao ni kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Jumuiya ya Ikizu (ICDT) siku ya tarehe 24/10/23 ofisini kwake.
Lengo la kikao hiko ni kukabidhi taarifa fupi inayoonyesha shughuli za Maendeleo watakazo zifanya kwa mwezi Disemba, 2023 na kuomba ridhaa kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji kushirikiana kwa pamoja katika shughuli hizo.
Mkurugenzi Mtendaji, Bi. Changwa M. Mkwazu akipokea taarifa kutoka kwa Mdau wa Maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, Bw. Juma Makonngoro
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0754335739
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda