Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mhe Lydia Bupilipili amewataka wafugaji wa Mifugo katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda kuchangamkia fursa ya chanjo ya mifugo iliyotolewa na Serikali kwa bei elekezi ya shilingi mia tano na hamsini(550).
Hayo yamesemwa wakati wa uzinduzi wa chanjo ya homa ya mapafu Mei 19,2021 katika Kijiji cha Sarakwa Kata ya Hunyari, Tarafa ya Chamriho.
Mhe Bupilipili alisema kuwa lengo la Serikali kuinua kipato cha wafugaji kutokana na kuuza mifugo na mazao yake iliyo bora ndani na nje ya nchi pamoja na kuinua uchumi wa nchi.
“Sekta ya mifugo ni sekta ya tatu katika kutupatia mapato katika nchi, hivyo ni vyema kwa wafugaji kuzingatia taratibu za ufugaji ili kuinua kipato cha mfugaji na nchi kwa ujumla’’alisema Bupilipili
Aidha Mhe Bupilipili ametoa rai kwa viongozi kuanzia ngazi ya kijiji na Halmashauri kuhakikisha wafugaji wote wanatekeleza agizo la kupeleka mifugo kupata chanjo na atakae kaidi hatua zaidi zichukuliwe.
“Kila kiongozi anawajibu wakuhakikisha kuwa zoezi hili linafanikiwa kwa asilimia mia na kwa mfugaji atakae kaidi hatua zaidi zichukuliwe’’.alisema Bupilipili
Kwa Upande wake Afisa mifugo,Bi Mary Luseke alisema kuwa zoezi la utoaji wa chanjo kwa mifugo dhidi ya magonjwa kipaumbele litafanywa na Wataalamu wa mifugo kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Bunda na kusimamiwa na Watalaamu kutoka wizara ya mifugo.
Bi.Luseke alibainisha magonjwa ya Kipaumbele kwa Mifugo ni Homa ya mapafu ya Ngo’mbe,Homa ya mapafu ya Mbuzi,Sotoka ya mbuzi na kondoo,Ugonjwa wa miguu na midomo,Chambavu,Kimeta,Mapele ya Ngozi,Ndigana kali,Bonde la Ufa,Kichaa cha Mbwa,Kideri,Kutupa Mimba na Sotoka.
Bi Luseke alieleza Zaidi kuwa chanjo itakayoanza ni ya Homa ya mapafu ya Ng’ombe
‘’Jumla ya Ng’ombe 131.250 wenye umri kuanzia miezi sita na kuendelea watachanjwa kwa Mwaka 2020/2021’’.alisema Bi Luseke
Naye,Mwenyekiti wa Kijiji cha Sarakwa Bwa. Giragu Nyamurunga kwa niaba ya Wafugaji alishukuru Serikali kwakuwajali wafugaji katika kuwapelekea chanjo ili kuimarisha Mifugo yao.
Halmashauri ya Wilaya ya Bunda ina jumla ya Ng”ombe ya 173,502 ambao wanatengemewa kuchanjwa kulingana na magonjwa ya kipaumbele na zoezi hili la utoaji chanjo kwa Ng’ombe litadumu takribani siku Kumi na Tano.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0754335739
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda