Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mhe Lydia Bupilipili amewapongeza na kuwashukuru wadau mbalimbali wanaochangia maendeleo katika Wilaya ya Bunda.
Hayo yamesemwa Juni 4,2021wakati wa hafla ya kutunuku vyeti kwa wadau wa maendeleo katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Bunda uliopo Bunda .
Mhe Bupilipili alisema kuwa tunzo hizi kwa wadau zipo katika nyanja mbalimbali ikiwemo elimu,Afya,Maji,ulinzi wa amani nakusimamia maswala ya ukatili ya kijinsia,Kupitia Taasisi na watu mbalimbali waliweza kushirikiana na Serikali katika kuleta maendeleo Wilaya ya Bunda.
"Katika kutambua hilo sisi kama serikali hatuna budi yakutothamini mchango wao katika kuleta maendeleo Wilaya ya Bunda".alisema Mhe. Bupilipili
Aidha Mhe Bupilipili alisema kuwa changamoto zinazowakabili wananchi zimetatuliwa na Serikali kushirikiana na wadau, ambao wamekuwa chachu katika kusukuma gurudumu la maendeleo hapa Bunda.
"Kwa mfano TANAPA, Grumet Fund na Taasisi nyingine wamesaidia kufanikisha shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwemo ujenzi wa vyumba vya madarasa,Zahanati bila kuwasahau PCI ambao wamekuwa wakihamasisha chakula mashuleni ,kutoa vitabu,mafunzo kwa walimu wa KKK ambapo kwa kiasi kikubwa imesaidia ufaulu kwa wanafunzi".alisema Mhe.Bupilipili
Naye ,Makamu Mwenyewe kiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Mhe Keremba Irobi amewashukuru wadau wa maendeleo kwa kutosita kuchangia pindi inapotokea serikali inauhitaji wa mchango wao.
"Wadau wa maendeleo wamekua mstari wa mbele katika kuleta maendeleo BundaTuwapongeze"alisema Mhe Irobi.
Kwa hatua ingine Mhe Irobi amemshukuru Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mhe. Ldyia Bupilipi kwakuendelea kuwaunganisha wadau mbalimbali pamoja na Serikali katika kuleta maendeleo Bunda.
Kwa upande wake,Yassin Ally Mkurugenzi wa Shirika la Kivulini kwa niaba ya wadau wengine alimshukuru Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mhe.Lydia Bupilipili kwakuendelea kutambua na kuthamini mchango wa wadau wa maendeleo na kuahidi kuendelea kushirikiana katika shughuli yeyote kuleta maendeleo Bunda.
Mwisho Mhe Bupilipili alivishukuru vyombo vya habari vya kijamii vinavopatikana Bunda kwa kuibua na kutoa taarifa mbalimbali za Wilaya ya Bunda.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0754335739
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda