Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara, Ndugu Gerald Kusaya siku ya tarehe 9/5/2024 alitembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi katika shule ya sekondari ya wasichana Mara, iliyopo katika kijiji cha Bulamba, Kata ya Butimba katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.
Katibu Tawala Mkoa wa Mara, akikagua viti na vitanda katika shule ya sekondari ya wasichana Mara.
Katika ziara hiyo, Ndugu Kusaya alikagua ukamilishaji wa jiko na majiko ya kupikia chakula cha wanafunzi, bwalo la kulia chakula, mabweni ya kulala wanafunzi na vyoo katika shule hiyo, pia, alimuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda kuhakikisha wanawasimamia mafundi na kuhakikisha wanaongeza kasi ya ujenzi ili kuweza kukamilisha miundombinu yote kwa wakati.
Ukaguzi wa jiko la kupikia pamoja na majiko
Ndugu Kusaya alikagua viti, meza, pamoja na vitanda vya wanafunzi na kumuagiza Muhandisi wa Halmashauri kuhakikisha anawasimamia mafundi ili kukamilisha mapema zaidi na pia, alisisitiza idadi ya viti, meza na vitanda iongezwe ili viweze kuendana na idadi ya wanafunzi watakaoletwa hapo mwezi wa Saba, 2024.
Aidha, Ndugu Kusaya alimuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, kuhakikisha wanachonga barabara zote zilizopo ndani ya shule hiyo, pamoja na kuhakikisha wanajenga uzio haraka ili kuongeza ulinzi na usalama kwa wanafunzi na mali zao.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0754335739
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda