Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mh. Dr. Vicent Anney alifanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda siku ya tarehe 23/10/2023.
Katika ziara hiyo Mh. Mkuu wa Wilaya alitembelea na kukagua chanzo cha Maji katika Kijiji cha Karukekere, ambapo Mwenyekiti wa Kijiji Bw, Daniel Peter Ngawa alimshukuru Mh. Mkuu wa Wilaya kwa kuja kutembelea na kukagua miradi iliyopo katika Kijiji chao.
Bw. Ngawa alimuomba Mh. Mkuu wa Wilaya kuwaletea umeme katika mradi huo wa maji kwani kwa sasa wamekuwa wakitumia jenereta katika kuendesha mradi huo ambao umekuwa ni gharama mno.
Mh. Mkuu wa Wilaya aliwaahidi kulifanyia kazi ombi hilo, hivyo alimuagiza Meneja wa TANESCO kuhakikisha katika bajeti yao ndani ya mwaka huu kuhakikisha wanaleta umeme katika mradi huo pamoja na Wanakijiji wengine.
Pia, alitembelea na kukagua Ujenzi wa shule ya msingi shikizi ya Nyamagusu iliyopo katika Kijiji cha Karukekere, ambayo imejengwa kwa ushirikiano na Wananchi.
Mh. Dr. Anney aliwapongeza kwa ushirikiano na umoja wao katika ujenzi huo wa shule, pia, aliwataka kuhakikisha wanamshirikisha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ili aweze kuwapatia Wataalamu wa Ujenzi na kuwapa ramani pamoja na vipimo sahihi katika ujenzi, ili waweze kujenga majengo yaliyoimara na yenye ubora.
Mh. Mkuu wa Wilaya pia, alitembelea na kukagua Ujenzi wa shule ya sekondari Karukekere, ambayo imejengwa kwa nguvu za wananchi, shule hiyo ya sekondari hadi sasa ina jumla ya majengo manne ambayo wanafunzi tayari wameanza kuyatumia, hivyo aliwataka Wananchi kuongeza nguvu zaidi katika ujenzi huo na kuhakikisha wanamalizia madarasa mengine ili kuweza kupokea wanafunzi mwakani 2024.
Pia, alitembelea na kukagua Ujenzi wa Jengo la kina mama la kujifungulia lililopo katika Zahanati ya Karukekere, ambalo limejengwa kwa nguvu za wananchi na aliwaahidi kuchangia kiasi cha Tshs Milioni Moja katika kukamilisha jengo hilo.
Katika miradi mingine aliyotembelea na kukagua ni Barabara ya Karukekere-Kenkombyo, ambapo alimuagiza Meneja TARURA kuhakikisha anashughulikia changamoto zilizopo katika Barabara na kuhakikisha Wanakijiji wanaitumia katika kipindi chote kwa mwaka mzima. Alitembelea na kukagua Ujenzi wa mradi wa Maji Ragata na pia alitembelea na kukagua shughuli za uendeshaji na matengenezo ya mradi wa Maji Bulamba.
Mkuu wa Wilaya alihitimisha ziara yake kwa kutembelea na kukagua maendeleo ya Ujenzi wa shule ya Mkoa ya Wasichana iliyopo katika Kijiji cha Bulamba, Kata ya Butimba na Ujenzi wa shule ya sekondari ilyopo katika Kijiji cha Ragata, Kata ya Kasuguti.
Ujenzi wa Shule ya Sekondari, iliyopo kijiji cha Ragata.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0754335739
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda