Chama cha walimu Tanzania (CWT), Wilaya ya Bunda siku ya tarehe 2/8/2025 walidhamini bonanza la michezo kwa watumishi wa Wilaya ya Bunda yenye majimbo matatu ambayo ni Jimbo la Mwibara, Bunda Mjini na Jimbo la Bunda, bonanza lililofanyika katika viwanja vya shule ya Sekondari Makongoro iliyopo kata ya Nyamuswa katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.
Katika bonanza Hilo, michezo mbalimbali ilichezwa ambayo ni mpira wa Pete, wavu,mpira wa mkono, mpira wa miguu, kuvuta kamba, kukimbiza kuku, kunywa soda na mingine mingi, lengo la kuandaa kwa bonanza la watumishi ni maandalizi ya kuelekea mashindano ya SHIMISEMITA yanayotarajiwa kuchezwa mkoani Tanga mapema mwezi wa Nane, 2025.
Mgeni rasmi katika bonanza Hilo alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Ndugu George S Mbilinyi, ambapo aliwashukuru CWT kwa kuweza kudhamini bonanza Hilo, na watumishi wote waliojitokeza kushiriki michezo hiyo.
Ndugu Mbilinyi, aliwaomba watumishi kuendelea kufanya mazoezi zaidi ili kuwa na nguvu ya kushiriki katika mashindano ya SHIMISEMITA, na pia alitoa zawadi kwa washindi walioshika nafasi ya kwanza hadi ya tatu, katika mchezo wa mpira wa miguu, Pete, mpira wa wavu na mpira wa mikono.
Naye, Kaimu Afisa michezo wa Halmashauri ya Bunda Mji, Ndugu Florian Cassian aliwashukuru wakurugenzi wote wa Halmashauri ya Mji wa Bunda na Bunda DC kwa kuweza kuwapa fursa watumishi ya kushiriki katika bonanza hili, kwani linasaidia kujenga Afya, mahusiano,baina ya watumishi.
Watumishi kutoka majimbo yote matatu waliwashukuru CWT pamoja na wakurugenzi wote kwa kuwezesha kufanyika kwa bonanza hili..
Ndugu Mbilinyi aliwahimiza watumishi na wananchi kujitokeza kwa wingi katika mapokezi ya MBIO za MWENGE ambao kimkoa tunatarajia kupokea tarehe 15/8/2025 katika Halmashauri ya Mji wa Bunda.
" Jitokeze kushiriki uchaguzi Mkuu wa mwaka, 2025 kwa Amani na Utulivu".
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika:
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda