
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, Ndugu, Oscar J. Nchemwa, siku ya tarehe 7/11/2025 alipokea boti mpya ambayo imenunuliwa kutoka kampuni ya Nile fishnet motors, yenye thamani ya Tshs Millioni 35.

Ndugu Nchemwa alisema, boti hiyo ilinunuliwa kwa fedha kutoka mapato ya ndani ya Halmashauri, ambapo ni boti ya pili sasa kununuliwa kwa mapato ya ndani ya Halmashauri.
Lengo kuu la kununua boti hii ni kwa ajili ya kufanya doria ndani ya ziwa Viktoria, kudhibiti uvuvi haramu, ukusanyaji wa ushuru wa mazao ya ziwani na pia, kutumika kama chombo cha uokoaji kwa wavuvi pindi wanapopata shida wakiwa ndani ya maji.

Boti hiyo ilikabidhiwa na mwakilishi wa kampuni ya Nile fishnet motors, ndugu Ismail Joackim Manae kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Ndugu, Oscar J. Nchemwa na kukaguliwa na shirika la wakala wa meli Tanzania ( TASAC ), ambalo linashughulikia ubora na uthibiti wa vyombo vya majini, ambapo waliridhishwa na ubora wa boti hiyo kwa kuhakikisha vitu vyote muhimu vinavyotakiwa kuwepo kwenye boti hiyo vipo, na uimara wa boti.

Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika:
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda