Muwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, ambaye ni Kaimu Mkuu wa kitengo cha Utamaduni, Sanaa na Michezo, Ndugu. Eustace Kabwogi siku ya tarehe 16/8/2025 alipokea vifaa vya michezo kutoka kwa mdau wa maendeleo Dkt. Masinde Bwire.
Dkt. Bwire alisema, lengo la kufadhili vifaa hivi kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda ni kuinua vipaji mbalimbali vilivyopo katika Halmashauri, kwa kuhakikisha Halmashauri kupitia Kitengo cha Utamaduni Sanaa na Michezo kinaunda timu kuanzia ngazi za vitongoji, vijiji hadi kata, hii yote ni kwa ajili ya kuwasaidia vijana wa kiume na kike walipo katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.
"Leo hii tumeanza na kata hii ya Namuhula kwa kuleta vifaa vya michezo, na ninawaahidi na kiwahakikisha nitaendelea kuwafadhili vifaa vingine vya michezo katika Kata zote zilizopo katika Jimbo hili la Mwibara, tunataka tuwe na mechi na mashindano ya Kila mwaka katika kuhakikisha tunawainua vijana waliopo katika Halmashauri." Alisema Dkt.Bwire.
Ndugu Kabwogi alimshukuru Dkt Bwire kwa vifaa ambavyo ameweza kuvileta katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, hususani katika Kata ya Namuhula, hivyo amemuahidi na kumuahikikishia kuvisimamia vifaa hivyo kwa kuhakikisha vinatunzwa na kuvisimamia vijiji na vitongoji kuhakikisha vinaunda timu ambazo zitaenda kuunda timu ya Jimbo.
Naye Mwenyekiti wa Kata ya Namuhula, kwa niaba ya wananchi wote alimshukuru mdau kwa kuweza kuwaletea vifaa hivyo na Mkurugenzi Mtendaji kukubali kufadhiliwa vifaa vya michezo katika Kata ya Namuhula, aliahidi kuhakikisha anavisimamia vitongoji vyote vilivyopo katika Kijiji chake kuhakikisha vinaunda timu zilizo imara kwa ajili ya kupata timu Moja ya Kijiji.
Ndugu Kabwogi alisema, vifaa vilivyopokelewa ni jozi 5 za jezi kwa wanaume, mipira 18 na viatu 11 ambavyo vitaenda kugawiwa katika Kila kitongoji na kijiji kilichopo katika Kata ya Namuhula kwa ajili ya kuanza maandalizi ya kuunda timu za vijiji.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika:
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda