Kikao cha tathimini ya lishe kwa robo ya nne kwa mwaka wa fedha 2024/2025 ngazi ya Halmashauri cha kupokea na kujadili taarifa mbalimbali kutoka divisheni na vitengo mtambuka vinavyoshirikiana na uhamasishaji wa lishe katika jamii, kimefanyika siku ya tarehe 4/9/2025 katika ukumbi mdogo wa Halmashauri uliopo Kibara Stoo.
Akiongoza kikao hicho, Mwenyekiti wa kikao ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Ndugu George S Mbilinyi, aliwasisitiza na kuwakumbusha divisheni na vitengo vinavyohusiana na masuala ya lishe, kuhakikisha wanahamasisha wananchi wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda kula vyakula vyenye lishe Bora ili kuondokana na kupunguza utapiamlo katika jamii.
" Mnapokuwa na mikutano na wananchi wenu huko hakikisheni ajenda ya lishe inasisitizwa, na sio kuishia kuhamasisha lishe shuleni tu, hata jamii zetu zinatakiwa zifahamu umuhimu wa kupata mlo kamili na ulio na lishe Bora, hapo ndio tutaweza kupunguza utapiamlo katika jamii nzima." Alisema.
Wananchi wamekuwa wakilima mazao mbalimbali lakini wengi wao unakuta hawali mlo kamili wanaishia kuuza kwa wengine huku utapiamlo ukiendelea kuongezeka katika jamii, hivyo ni jukumu letu sote kuhakikisha tunashirikiana kwa pamoja kuhakikisha elimu inatolewa kwa wananchi wote kuhusiana na faida za kutumia vyakula vilivyo na viritubishi kwa ajili ya kupata lishe iliyo Bora.
Ndugu Mbilinyi, alimuagiza Afisa kilimo kwa kushirikiana na Afisa Biashara kuhakikisha wanawatafutia wakulima soko la kueleweka kwa ajili ya kuuza mazao yao, hasa mazao ya bustani ambayo yameonekana wakulima wamekuwa wakilima lakini hawana soko la uhakika la kupeleka mazao yao hivyo kupelekea kukata tamaa kwa wakulima kuendelea kulima mazao hayo.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika:
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda