Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, kupitia kitengo cha huduma za Sheria siku ya tarehe 9/7/2025 kiliwajengea uwezo wa namna ya kusuluhisha migogoro ya ardhi katika Kata.
Mkuu wa kitengo cha huduma za Sheria wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, Bi. Scola Kisibo aliwasomea mwongozo wa usuluhishi wa migogoro ya ardhi katika mabaraza ya kata, ambapo, alisema kazi ya mabaraza ya kata ni kusuluhisha tu na sio kutoa hukumu katika malalamiko yatakayowasilishwa kuhusiana na migogoro ya ardhi katika Kata, pia, alisema migogoro hiyo ni lazima iwe ndani ya kata husika na ihusishe mlalamikaji na mlalamikiwa katika uwasilishwaji wa malalamiko hayo.
Aliwasomea sifa za kuwa mjumbe wa Baraza la kata, na kusema muda wa kuhudumu ndani ya Baraza la kata ni miaka mitatu, na baada ya hapo watachagua wajumbe wengine wapya au kuwarudisha watakaokuwa na sifa.
" Mtu hatachaguliwa kuwa mjumbe wa Baraza la kata endapo atakosa sifa hizi:, kama sio raia wa Tanzania, akiwa na umri wa chini ya miaka 18, akiwa Mtumishi wa umma, au akiwa mjumbe wa Baraza la ardhi la Kijiji, Halmashauri ya Kijiji au kamati ya Maendeleo ya kata, mwanasheria au mtu yeyote aliyeajiriwa na mahakama, Mbunge, au kama amewahi kutiwa hatiani kwa kosa lolote la jinai." Alisema Bi. Kisibo.
Mwanasheria aliwasomea mambo muhimu yanayotakiwa kuzingatiwa katika mabaraza hayo wakati wa usuluhishi na hatua za kufuata katika usuluhishi.
Wajumbe walishukuru na kupongeza kitengo cha Sheria kwa kuweza kuwajengea uwezo katika usimamizi na uendeshaji wa mabaraza ya kata hususani katika usuluhishi wa migogoro ya ardhi ndani ya kata, kwani itawasaidia kutatua migogoro itakayokuwa inajitokeza ndani ya kata zao mapema zaidi.
Mafunzo ya wajumbe wa mabaraza ya kata yalitolewa katika Kata ya Nyamuswa na Nyamang'uta, katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika:
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda