Msimamizi wa uchaguzi wa serikali za mitaa Bw. George S. Mbilinyi siku ya tarehe 26/9/2024 ametoa maelezo kwa umma kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa,2024 katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, uliopo Kibara Stoo.
Mkutano huo ulishirikisha viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wazee maarufu, wakuu wa divisheni na vitengo kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.
Bw. Mbilinyi aliwasilisha maelezo muhimu kuhusiana na uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika tarehe 27/11/2024.
Msimamizi Msaidizi wa uchaguzi Bw. Modestus Chama alisema, uchaguzi wa serikali za mitaa unafanyika katika vitongoji, kila mtu anapaswa kwenda kujiandikisha kupiga kura katika kitongoji chake kwa ajili ya kuwachagua viongozi walio bora kwa ajili ya kushirikiana nao katika kijiji na kitongoji kuhakikisha wanaleta maendeleo chanya.
“hivyo kila mtu mwenye sifa ya kupiga kura atapiga kura katika kitongoji kimoja kuwachagua viongozi husika, na katika kitongoji kimoja.” Alisema Bw. Chama.
Wajumbe waliohudhuria mkutano huo walimshukuru Msimamizi wa uchaguzi kwa kuwaalika kwa ajili kuja kupokea maelezo hayo muhimu ya uchaguzi wa serikali za mitaa, waliahidi kwenda kutoa elimu katika jamii na kuwahamasisha wananchi kwenda kujiandikisha siku itakapofika na kushiriki katika uchaguzi unaokuja.
Msimamizi wa uchaguzi aliwashukuru wajumbe wote waliohudhuria mkutano huo, aliwaomba viongozi wa dini, wazee maarufu, na viongozi wa vyama vya siasa kuhakikisha wanaenda kutoa elimu na kuwahamasisha wananchi kujitokeza katika uandikishaji wa wapiga kura siku ya tarehe 11 hadi 20 ya mwezi wa kumi, 2024 na kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa,tarehe 27/11/2024.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0754335739
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda