Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, Ndugu George S. Mbilinyi siku ya tarehe 2/7/2024 alipokea boti mpya ambayo imenunuliwa kutoka kwenye kampuni ya Nile Fishernet Motors CO. LTD.
Boti aina ya fiber glass ambayo ni maalumu kwa ajili ya doria ziwani, imenunuliwa kwa mapato ya ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Bunda kwa kiasi cha Tshs 62,314,000 (Millioni Sitini na Mbili Laki tatu na Elfu Kumi na Nne).
Ndugu Mbilinyi alisema, lengo kuu la manunuzi ya boti hii ni kwa ajili ya kufanya doria ndani ya ziwa Victoria kwa ajili ya ukusanyaji wa mapato na kudhibiti uvuvi haramu. Hivyo aliwataka maafisa uvuvi kuhakikisha wanaitunza na kuitumia kwa kazi husika ili kuongeza mapato ya Halmashauri.
Naye, Afisa Uvuvi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, Ndugu Peter Sweke alimshukuru Mkurugenzi Mtendaji kwa kuweza kuwanunulia boti hiyo ambayo itasaidia katika ukusanyaji wa mapato kwa upande wa ziwani.
Boti hiyo ambayo imepewa jina la MV CHANGWA ina uwezo wa kubeba abiria 15.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda