• Malalamiko |
    • Maswali |
    • Barua Pepe |
Bunda District Council
Bunda District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Kilimo, Umwagiliaji & Ushirika
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji
      • Fedha & Biashara
      • Ujenzi
      • Afya
      • Mifugo & Uvuvi
      • Elimu Sekondari
      • Rasilimali Watu
      • Maendeleo ya Jamii
      • Usafi & Mazingira
      • Elimu Msingi
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ufugaji Nyuki
      • Uchaguzi
      • Manunuzi
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Elimu Msingi
    • Barabara
    • Mifugo
    • Afya
    • Mazao ya kilimo
  • Fursa za Uwekezaji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha, Uongozi & Mipango
      • Elimu, Afya & Maji
      • AIDS Control
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taarifa
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Uma
    • Video
    • Hifadhi ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mhe Lydia Bupilipili aongoza Kikao cha Wadau wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini(RUWASA)

Posted on: August 29th, 2020

Wakala wa Maji  Usafi wa mazingira Vijijini imefanya  mkutano wa Mwaka  wa Pilli wa Sekt na Wadau wa  Maji na Usafi wa mazingira 28Agosti,2020 katika ukumbi wa Malaika uliopo Bunda Mji, lengo  la majadiliano ni kuwa nauelewa wa pamoja kuhusu maendeleo ya Sekta  ya  Maji katika Wilaya ya Bunda kwa ujumla.

Akifungua Mkutano huo mkuu wa Wilaya ya Bunda Mhe.Lydia Bupilipili amesema anawapongeza Wizara ya Maji kupitia RUWASA Ngazi ya Mkoa na Wilaya kwa kuweka utaratibu wa  kuwepo kwa mkutano wa wadau ambapo unasaidia kutambua wapi tulipo toka,wapi tulipo na wapi tunakwenda na hii ni chachu ya maendeleo kwa jamii inayotunguka kwakuweza kutatua changamoto za maji kwa jamii kupitia vikao hivi.

“utaratibu wa vikao vya wadau wa maji ni muhimu  husaidia kutambua changamoto mbalimbali na hata kujua nani anakwamisha  katika kuleta maendeleo  kwa jamii kupitia maazimio ya  yanatolewa katika kikao”.alisema Mhe Bupilpili

Mhe Bupilipili amesema kuwa huduma ya maji  katika maisha ya Mwanadamu halikwepeki, uwepo wa maji ya  uhakika  katika jamii husaidia kufanya Wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo ya jamii, hivyo ni muhimu kila mmoja wetu kuwajibika kwa nafasi yake ili kuondoa  na kuimaliza changamoto ya  maji katika jamii.

“kama serikali ni jukumu letu kuhakikisha  kuwa wananchi wanapata maji safi na salama”.

Aidha Bupilipili ametoa  wito kwa viongozi wa serikali ya vijiji kutobadilisha matumizi ya fedha za miradi ya maji kupeleka katika miradi mengine kwani kufanya hivo ni kuendelea kufanya akina mama wateseke kufuata maji umbali mrefu.

“kila kiongozi ni jukumu lake kuleta hamasa kwa wananchi kushiriki katika miradi ya maendeleo itasaidia kutobadilisha matumzi ya pesa za miradi ya  maji kutumika katika miradi mengine”.

Naye Kaimu Meneja RUWASA Bunda Eng. Lucas N.Madaha amesema kuwa  Serikali imetoa  kiasi cha Bilioni 1.3 za kutekeleza miradi ya maji ambayo itachangia kuondoa na kupunguza changamoto ya maji.katika maeneo mbalimba hapa Bunda.

“Fedha hizi zimeletwa na serikali kwaajili ya Wananchi wake  ili wasipate tabu kutembea umbali mrefu wa  kufuata maji hasa akina mama”.alisisitiza Eng.Madaha

Aidha Eng  Madaha amesema kuwa Serikali inafanya mengi  katika kuhakikisha kuwa inapata maji katika vyanzo vilivyoboreshwa  jumla  ya shiilingi Bilioni 6 zimeekezwa katika kipindi cha Serikali ya awamu tano chini Dkt John pombe Magufuli katika kuboresha huduma ya maji.

“Hivyo wadau wa maji ni muhimu kuelewa uchangiaji na kulinda miundombinu ya huduma ya maji ili iwe endelevu”.

Halmashauri ya Wilaya ya Bunda ni moja kati ya Halmashauri 87 zilizonufaika na mradi  wa maendeleo endelevu ya Maji vijijini(Rural Water Supply and Sanitation Program) ikiwa huduma ya maji imeongezeka kutoka asilimia 43.5 mpaka asilimia  68.9 .

Matangazo

  • FOMU YA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA KATIKA SHULE YA SEKONDARI SALAMA December 17, 2020
  • FOMU YA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA KATIKA SHULE YA SEKONDARI MWIBARA December 17, 2020
  • FOMU YA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA KATIKA SHULE YA SEKONDARI CHITENGULE December 17, 2020
  • FOMU YA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA KATIKA SHULE YA SEKONDARI MURANDA December 17, 2020
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • Shule za Msingi,Mugeta,Sanzate na Nyamitwebili zilipo Halmashauri Wilaya ya Bunda yanafuika na jengo la Maktaba yaliyofadhiliwa na Shirika lisilo la Serikali PCI

    December 19, 2020
  • Halmashauri Ya Wilaya ya Bunda ya Zindua Mkutano wa Kwanza wa Baraza la Madiwani.

    December 17, 2020
  • Halmashauri ya Wilaya ya Bunda,Butiama ,Serengeti na Musoma Dc yanufaika na Mafunzo ya TARI

    December 05, 2020
  • Halmashauri ya Wilaya ya Bunda yaadhimisha siku ya Ukimwi Duniani.

    December 04, 2020
  • Angalia zote

Video

Mvamizi wa eneo la soko.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Baraza la Madiwani
  • Dira na Dhamira
  • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Mpango Mkakati
  • Mpango wa Uwekezaji Sekta ya Samaki
  • Muundo wa Taasisi
  • OPRAS - Form

Viunganishi Muambata

  • Matokeo ya Darasa la Saba 2020 Bundadc
  • Matokeo ya Kidato cha Nne 2019
  • Sekretarieti ya Ajira
  • PO-RALG
  • PO-PSM
  • Mara Secretariet

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Kilimani Street

    Anuani ya Posta: 126, Bunda

    Simu: 0677002976

    Hamishika: 0783669938

    Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda