Mwenyekiti wa kamati ya Ushauri ya Wilaya ya Bunda (DCC) Ndugu Salum Khalfani Mtelela kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Bunda amewataka wananchi wa Wilaya ya Bunda kuchukua tahadhari juu ya ugonjwa wa kipindupindu ambao umekuwa na madhara makubwa kwa siku za hivi karibuni.
Ameyasema hayo katika kikao cha kamati ya Ushauri ya Wilaya ya Bunda kilichofanyika siku ya tarehe 3/03/2025 katika ukumbi wa Halmashauri ya Bunda Mji, lengo kuu la kikao hicho likiwa ni kujadili na kupitisha rasimu ya mpango na bajeti kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
“Mpaka sasa kuna baadhi ya wananchi wamekumbwa na ugonjwa huo hasa katika kata ya Igundu hivyo amewaagiza viongozi wa kata kuchukua hatua ikiwemo kuwahimiza wananchi kuchimba vyoo, kunawa mikono kwa maji safi na sabuni kabla na baada yakula, kusitisha sherehe zisizo za msingi pamoja na kuimarisha usafi wa mazingira.”Amesema
"Watu wa afya chukueni hatua kulingana na taratibu za kiafya, mtu yeyote au kiongozi yeyote anayejaribu kuzuia juhudi za kupambana na ugonjwa huu toeni taarifa ili tumuchukulie hatua za kisheria kwasababu kumekuwa na baadhi ya viongozi wa serikali wamekuwa wakiwapotosha wananchi juu ya ugonjwa huu kutokana na Imani zao potofu."Amesema Ndugu Mtelela
Aidha, Ndugu Mtelela amewataka wananchi kutotumia dhana ya elimu bure na kushindwa kuchangia chakula cha wanafunzi shuleni na kuwataka wachangie ili wanafunzi wote waweze kupata chakula shuleni kwani itasaidia kuongeza ufaulu wa wanafunzi.
"Kuna baadhi ya wananchi wamekuwa wakishindwa kuchangia chakula cha wanafunzi shuleni kwa kusingizia kuwa walimu wanakula chakula hicho hali inayorudisha nyuma jitihada za serikali za kuhakikisha kila mwanafunzi anapata chakula anapokuwa shuleni ili kuongeza ufaulu wa wanafunzi hao"amesema Katiba Tawala
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda