Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Ndugu George S Mbilinyi siku ya tarehe 14/8/2025 amewaaga rasmi watumishi wanaoelekea mkoani Tanga kwa ajili ya kushiriki kwenye mashindano ya SHIMISEMITA, yanayotarajiwa kuanza rasmi tarehe 15/8/2025.
Akizungumza na watumishi hao, amewataka kuwa na ushirikiano na kuhakikisha wanakuwa na nidhamu katika michezo hiyo na kuhakikisha wanarudi na ushindi nyumbani.
" Tunatarajia mtarudi na vikombe vya ushindi katika mashindano hayo na sio kwenda kushiriki tu, hivyo mnatakiwa muwe na ushirikiano wakati wote mnapokuwa uwanjani, maana ninaamini mmefanya mazoezi ya kutosha na mmejiandaa vyema kurudi na ushindi" alisema Ndugu Mbilinyi.
Naye, kapteni wa mpira wa miguu kwa wanaume Ndugu, Mohammed Jumanne alimshukuru Mkurugenzi Mtendaji kwa kuwawezesha kwenda kushiriki katika mashindano hayo, na hivyo alimuahidi na kumuhakikishia kwamba watarudi na ushindi kwani wamefanya mazoezi ya kutosha kwa ajili ya kujiandaa na mashindano hayo.
Pia, aliwasihi wachezaji wenzake kuhakikisha kwamba wote wanakwenda kupambana katika mashindano hayo na kurejea na ushindi nyumbani.
Jumla ya wachezaji 27 wanaenda kushiriki mashindano hayo ikiwa 17 ni wanaume kwenye michezo wa mpira wa miguu na 10 ni timu ya wanawake ambao watashiriki mpira wa Pete.
"Jitokeze kupiga kura kwa maendeleo ya Michezo."
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika:
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda