Timu ya wataalamu tathimini na ufuatiliaji kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Bunda siku ya tarehe 26/3/2025 wamefanya ziara ya siku mbili ya kutembelea na kukagua miradi ya Maendeleo kwa upande wa Afya na elimu inayoendelea kutekelezwa katika Halmashauri.
Lengo la ziara hiyo ni kufanya tathmini na kufuatilia fedha zilizotolewa kupitia Mfuko wa Jimbo na mapato ya ndani katika miradi ya Afya na elimu zimefikia wapi katika utekelezaji wa miradi hiyo tangu walipozipokea katika akaunti zao kwa ajili ya utekelezaji.
Timu hiyo, ilitembelea na kukagua hospitali ya Wilaya ambayo ilipokea fedha za mapato ya ndani, zikiwa na lengo la kusambaza umeme kwenye majengo 12 katika hospitali ambapo tayari hatua za Awali zimeshaanza kutekelezwa ikiwemo hatua za manunuzi kupitia mfumo wa Nest.
Pia, walitembelea shule ya msingi Songambele, Salama B, Kabainja, Sarawe, Nyamuswa A, ujenzi wa matundu 10 ya vyoo katika shule ya Sekondari Nansimo, ukamilishaji wa jengo la ofisi ya Kata Salama.
Miradi hii baadhi imepokea fedha kutoka Mfuko wa Jimbo na mapato ya ndani kwa ajili ya utekelezaji na ukamilishaji.
Timu ya wataalamu ya tathmini na ufuatiliaji wa miradi walitembelea na kukagua Zahanati ya Kyandege, Mwiseni, Muranda, Nyamitwebili, Tiringa'ati na Kabainja. Zahanati hizi zimepokea fedha kutoka mapato ya ndani kwa ajili ya utekelezaji na ukamilishaji.Miradi hiyo yote imepokea fedha za Mfuko wa Jimbo na mapato ya ndani kwa ajili ya ujenzi na ukamilishaji, hivyo timu ilipita kukagua na kujiridhisha kama fedha zilizopokelewa zipo katika hatua Gani ya utekelezaji katika miradi na kuwasisitiza wasimamizi wote wa miradi kuharakisha utekelezaji wake haraka ili miradi iweze kukamilika kwa wakati na wananchi waweze kupata huduma kama zilivokusudiwa.
Katika miradi yote waliyotembeleatay baadhi ya miradi ilikuwa imeshaanza utekelezaji wake na wapo hatua mbalimbali za ununuzi wa vifaa na ukamilishaji ili kuweza kukamilisha kabisa miradi.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda