Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Bunda Ndugu Juma Chikoka aliwaagiza watendaji wa KATA na MIJI kuendelea kuweka msisitizo katika maeneo ambayo badouchangiaji wa chakula shuleni ni hafifu.
Agizo Hilo alilitoa siku ya tarehe 8/9/2025 katika kikao cha tathimini ya lishe kwa robo ya nne kwa mwaka 2024/2025, kilichofanyika katika ukumbi wa mkutano wa Halmashauri ya Bunda Mji.
" Ajenda hii ya lishe ni ya Kitaifa na ni jukumu letu kuhakikisha tunafikia malengo yaliyokusudiwa, Kila Mmoja kwa nafasi yake ahakikishe anatimiza majukumu yake, wakurugenzi na wataalamu mnatakiwa mshuke ngazi za chini kwa ajili ya kuongeza uhamasishaji na elimu kwa wananchi katika uchangiaji wa chakula shuleni." Alisema Ndugu Chikoka.
Ndugu Chikoka aliwaagiza wakurugenzi kuhakikisha wanaweka utaratibu wa kubaini na kutambua motisha kwa watendaji wanaofanya vizuri katika kuhamasisha jamii inachangia chakula shuleni.
"Maafisa elimu mkishirikiana na maafisa lishe hakikisheni mnashirikiana kwa pamoja katika kuhakikisha mnayasimamia mashamba ya shule ili yatumike vizuri kwa kuhakikisha yanaleta tija na matokeo chanya kwa wanafunzi. Wataalamu ngazi ya Kata na MIJI watumike ipasavyo katika kuhakikisha wanahamasisha uchangiaji wa chakula shuleni." Aliagiza Ndugu Chikoka.
Ndugu Chikoka alihitimisha kikao hicho kwa kuagiza sote pamoja twendeni tukafanye KAZI kwa bidii ili kuleta mabadiliko katika ajenda hii ya lishe.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika:
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda