Mafunzo ya mfumo wa FFARS yametolewa kwa watumishi ngazi za vituo katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, ambapo yalihusisha watumishi wa Afya, elimu, watendaji wa kata na vijiji.
Mafunzo hayo ya siku 5 yalifanyika katika shule ya Sekondari ya wasichana Mara, yalihitimishwa siku ya tarehe 9/9/2025.
Mratibu wa mafunzo hayo, Ndugu Jacob Jeconia ambaye ni Afisa Hesabu wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, alisema lengo la mafunzo haya ni kwa ajili ya kufundishana na kuelezana kanuni, Sheria na taratibu za kufuata wakati wa kufanya manunuzi kupitia mfumo wa Nest.
Ndugu Jeconia alisema, mfumo wa FFARS ni mfumo wa uhasibu na utoaji taarifa za fedha kwa ngazi za vituo vya kutolea huduma. Mfumo huu unasaidia kuleta uwazi, uwajibikaji na uwezeshaji wa utoaji taarifa za mapokezi ya fedha na matumizi yakiwepo na malipo mbalimbali yaliyofanyika.
Lengo la maboresho haya ni kwa ajili ya kuondoka matumizi ya hundi, ambapo kupitia mfumo huo unaweza kuandika hundi ya malipo kwenda kwa mlipwaji, pia kupitia mfumo huu unatakiwa kupata kibali cha kuomba kutumia fedha kwa matumizi mbalimbali.
Ndugu Jeconia alisema maboresho yamefanyika katika maeneo yafuatayo, ambayo ni
- Eneo la kuhuisha akaunti ya mteja.
-Eneo la kufanya mahamisho ya fedha zako.( Allocation).
- Eneo la kuomba kibali cha malipo, pamoja na Eneo la kuandaa hati ya malipo( risiti).
" Kibali cha kuombea fedha lazima kiwe na maelezo ya kujitosheleza kabla hakijatumwa kwa Afisa masuhuli kwa ajili ya kukiidhinisha.
Naye, Mkaguzi wa ndani wa Halmashauri Bi. Florence Kaluretele aliwaambia washiriki hao wa mafunzo kuhakikisha wanapopokea mahitaji kutoka kwa mzabuni kukagua kama yapo sahihi na wahakikishe wanakagua na risiti kuhakikisha zipo sawa ili kuepusha migogoro isiyo na tija.
Afisa Elimu Sekondari, Bi. Pendo Masalu aliwashukuru ofisi ya fedha na uhasibu kwa kuwezesha mafunzo hayo kwa wakuu wa shule na wahasibu katika matumizi ya mfumo huu wa FFARS ulioboreshwa ambao unatumika katika kufanya malipo mbalimbali katika vituo vyao vya kazi.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika:
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda