Tangu kuzinduliwa rasmi kwa Baraza la wazee katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda siku ya tarehe 15/6/2023, katika Kata ya Mugeta, kwa mara ya kwanza Halmashauri ya Wilaya ya Bunda imefanya kikao cha Baraza la wazee kwa kuwaalika viongozi wa ngazi mbalimbali kuanzia Kijiji, kata hadi Halmashauri kwa niaba ya wazee wote waliopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.
Afisa ustawi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, ambaye ni Mratibu wa huduma za wazee Bi. Neema Milanzi alisema, lengo la kuitisha kikao hiki ni kwa ajili ya kuwasomea muongozo wa Kitaifa wa uanzishwaji na uendeshaji wa mabaraza ya ushauri ya wazee.
Kufahamu, majukumu ya viongozi waliochaguliwa katika mabaraza ya ushauri ya wazee ambayo yanaanzia ngazi za vijiji, kata, hadi Halmashauri, sifa za kuwa kiongozi katika mabaraza hayo ya ushauri ya wazee.
Bi. Milanzi pia, alielezea idadi ya vikao kisheria vinavyotakiwa kufanyika katika mabaraza hayo kuwa ni vinne kwa mwaka, na ukomo wa kuwa kiongozi katika mabaraza hayo ni miaka mitano, ndio uchaguzi mwingine utafanyika kwa ajili ya kuchagua viongozi wapya.
Afisa ustawi alieleza sababu zinazopelekea ukomo wa kuwa kiongozi katika mabaraza hayo ikiwemo kifo.
Katika kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri siku ya tarehe 3/7/2025, Bi. Milanzi alisoma taarifa ya huduma za wazee, mafanikio, changamoto, na utatuzi wake katika kuhakikisha wanaboresha mabaraza yote ya ushauri ya wazee kwa ngazi zote.
Aidha, katika kikao hicho wajumbe waliweza kupokea mrejesho wa maadhimisho ya siku ya wazee Duniani Kitaifa yaliyofanyika Tabora na Shinyanga kutoka kwa Mzee. Range Chacha.
Wawakilishi hao wa wazee, walishukuru kwa kufanyika kwa kikao hicho kwa mara ya kwanza tangu walipozindua Baraza lao, pia waliwasilisha changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo kwa upande wa kupata huduma za matibabu, na upande wa taasisi za mikopo kuwanyima mikopo kwa kisingizio cha uzee.
Muwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji, ambaye ni Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, Ndugu Bruno Yulop aliwapongeza viongozi hao na aliwashukuru kwa kuweza kuhudhuria kikao hicho.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika:
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda