Kamati ya huduma za jamii ya Halmashauri ya Wilaya ya Bunda kwa kushirikiana na wataalamu kutoka Halmashauri,wamefanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya Afya na Elimu inayotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, siku ya tarehe 21/1/2025.
Ziara hiyo imeongozwa na Kaimu Mwenyekiti wa kamati ya huduma za jamii ambaye pia ni diwani wa kata ya kibara Mhe.Mtamwega Toto Mgaywa na lengo kuu la ziara ni kutembelea na kukagua maendeleo ya miradi inayotekelezwa katika kipindi cha robo ya pili kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
Wajumbe wa kamati walitembelea na kukagua miradi ya elimu ambapo,walitembelea shule ya msingi Namibu A na kukagua ukamilishaji wa vyumba vitatu vya madarasa na matundu sita ya vyoo,pia, walitembelea na kukagua ujenzi katika shule ya msingi Bulomba ambapo walikagua vyumba vinne vya madarasa ya msingi na awali pamoja na matundu 12 ya vyoo.
Pia, walitembelea shule ya msingi Igundu na walikagua ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa na matundu sita ya vyoo na ujenzi upo katika hatua ya ukamilishaji wa lipu.
Miradi hiyo ya elimu msingi na awali ni fedha kutoka serikali kuu kupitia mradi wa Boost.
Aidha, kamati ilitembelea na kukagua ujenzi wa shule mpya ya sekondari ya Amali, iliyopo kijiji cha Makwa kata ya Nampindi ambapo jumla ya majengo 11 yanajengwa katika shule hiyo.
Kamati ilikagua ukamilishaji wa nyumba ya Mwalimu (2 in1) ambayo ipo katika hatua ya upauaji, pia,walikagua ujenzi wa majengo yanayoendelea kujengwa katika shule hiyo ambayo yapo katika hatua za ufungaji wa lenta,ujenzi wa msingi na upauaji.
Pia walitembelea na kukagua shule mpya ya sekondari Mahyolo iliyopo katika kijiji cha Mayolo ambapo, ujenzi wake upo katika hatua za ufungaji wa lenta na ujenzi wa msingi.
Kamati ya huduma za jamii ilihitimisha ziara yake kwa kutembelea na kukagua ukamilishaji wa Zahanati ya Mwiseni iliyopo kata ya Butimba.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0742163056
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda