Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Ndugu George S Mbilinyi siku ya tarehe 26/6/2025 amefanya ziara ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa hospitali ya Wilaya iliyopo Kijiji cha Bukama.
Katika ziara hiyo, Ndugu Mbilinyi alitembelea na kukagua ujenzi wa njia za kutembelea wagonjwa, ambao unaendelea kutekelezwa katika hospitali, pia alitembelea na kukagua ukamilishaji wa jengo la wodi ya wanaume, wanawake na watoto.
Aidha, katika ziara hiyo, Ndugu Mbilinyi alitembelea kata ya Salama na kuzungumza na watumishi wote wanaoishi kata ya Salama, lengo kuu la kutembelea kata hiyo ni ufuatiliaji wa maagizo na mikakati waliyopewa kuona kama yametekelezwa kama walivyoagizwa.
Mtendaji wa kata ya Salama, Ndugu Ruben Maduhu aliwasilisha taarifa ya utekelezaji katika Kata, ambapo, aliwasilisha taarifa ya idadi ya majengo yote yaliyopo katika Kata, ambayo yanasifa ya kusajiliwa na yasiyokuwa na sifa ya kusajiliwa kwa ajili ya kuanza kutozwa Kodi.
Pia, aliwasilisha taarifa ya maduka yote yaliyopo katika Kata ya Salama, ambayo yameshakata leseni ya biashara na ambayo hayajakata leseni za biashara, taarifa ya watumishi waliopo katika Kata ya Salama, na taarifa za idara zilitolewa na watumishi husika.
Ndugu Mbilinyi alimuagiza Mtendaji wa Kata kuhakikisha anawasimamia watendaji wote wa vijiji kuhakikisha wanasajili majengo yote yenye sifa katika vijiji na vitongoji vyao ndani ya siku Saba wawe wameshakamilisha na kupata mrejesho.
Kwa upande wa maduka, Ndugu Mbilinyi, alimuagiza Afisa biashara wa Halmashauri Ndugu. Samweli Werema kuhakikisha wanashirikiana na Mtendaji wa kata kuhakikisha hadi ifikapo tarehe 30/6/2025 maduka yote ambayo hayana leseni ya biashara wahakikishe wameshakata na kupata leseni hizo.
" Watumishi wote wanaoishi nje ya maeneo ya kazi, wahakikishe wanahamia na kuishi katika maeneo yao ya kazi". Aliagiza Mkurugenzi Mtendaji.
Taarifa ya idara kilimo katika Kata ya Salama iliwasilishwa na Afisa kilimo, Bi. Experansia Nyaonge., na taarifa ya idara ya Afya iliwasilishwa na Waganga wafawidhi katika zahanati wanazozisimamia.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika:
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda