• Malalamiko |
    • Maswali |
    • Barua Pepe |
Bunda District Council
Bunda District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Kilimo, Umwagiliaji & Ushirika
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji
      • Fedha & Biashara
      • Ujenzi
      • Afya
      • Mifugo & Uvuvi
      • Elimu Sekondari
      • Rasilimali Watu
      • Maendeleo ya Jamii
      • Usafi & Mazingira
      • Elimu Msingi
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ufugaji Nyuki
      • Uchaguzi
      • Manunuzi
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Elimu Msingi
    • Barabara
    • Mifugo
    • Afya
    • Mazao ya kilimo
  • Fursa za Uwekezaji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha, Uongozi & Mipango
      • Elimu, Afya & Maji
      • AIDS Control
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taarifa
    • Sheria Ndogo
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Uma
    • Video
    • Hifadhi ya Picha
    • Habari
    • Matukio

ZIARA YA MKUU WA WILAYA YA BUNDA KUTEMBELEA NA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO

Posted on: April 24th, 2024

Katika kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amewezesha ujenzi wa bweni la watoto wa kike wenye mahitaji maalumu katika shule ya msingi Nansimo, iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.

Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Mh. Dkt Vicent Anney siku ya tarehe 23/4/2024 alifanya ziara ya kutembelea na kukagua bweni hilo ili kuona hatua ilipofikia, katika ziara yake Mh. Mkuu wa Wilaya aliongozana na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya, TARURA, TANESCO, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, pamoja na baadhi ya wakuu wa idara kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.

Dkt Anney alisema, mradi huu unatakiwa uwe na tija kwa wananchi wote wa Kata ya Nansimo na maeneo ya jirani, kwani hii ni zawadi ya pekee aliyoitoa Mh. Rais katika maadhimisho haya ya miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hivyo mnatakiwa muhakikishe mnausimamia vyema ili uweze kukamilika kwa wakati uliopangwa na kuwasaidia watoto wetu wenye mahitaji maalumu kuweza kupata elimu katika mazingira yaliyo rafiki.

Akisoma taarifa ya mradi wa ujenzi Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Nansimo, Bi. Jane Nsinwa alisema mradi huu unafadhiliwa na fedha kutoka serikali kuu, ambapo walipokea kiasi cha Tshs Million 128, na hadi sasa ujenzi ulipofikia wameshatumia kiasi cha Tshs Million 44,326,000/= na ujenzi upo hatua ya umwagaji wa jamvi, na unatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2024.

Mkuu wa Wilaya alimpongeza Diwani wa Kata ya Nansimo, Mh. Edward Justas Namwatta, viongozi na wananchi wa kijiji cha Nansimo kwa usimamizi wao mzuri  katika ujenzi wa mradi huo, hivyo aliwaagiza kuhakikisha wanawasimamia mafundi ili kuweza kukamilisha mradi kwa wakati.

“Mradi kwa ujumla unaendelea vizuri sana hadi hapa ulipofikia, ongezeni juhudi katika kuhakikisha mnawasimamia mafundi wote wanaojenga hapa ili kukamilisha kwa wakati, na hongereni sana.” Alisema Dkt. Anney.

Pia, alitembelea na kukagua ukamilishaji wa zahanati mbili zilizopokea kiasi cha Tshs Million 50 kila moja kutoka serikali kuu, ambazo ni zahanati ya Mwiseni na Nambaza. Katika zahanati ya Nambaza alipongeza kwa ujenzi mzuri unaoendelea na aliagiza kufanyika marekebisho kwa baadhi ya maeneo yaliyokuwa na changamoto na kuhakikisha mafundi wanamalizia ukamilishaji wa zahanati hiyo ili iweze kufunguliwa mapema na wananchi waweze kupata huduma ya Afya kwa ukaribu.

Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAILI October 11, 2025
  • KUITWA KWENYE USAILI October 11, 2025
  • TANGAZO LA MIKOPO October 01, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI August 27, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • WATUMISHI NGAZI ZA VITUO WAPEWA MAFUNZO YA MFUMO WA FFARS ULIOBORESHWA

    September 10, 2025
  • WATENDAJI KATA NA MIJI WAAGIZWA KUENDELEA KUWEKA MSISITIZO KATIKA UHAMASISHAJI WA UCHANGIAJI WA CHAKULA SHULENI

    September 09, 2025
  • HALMASHAURI YAADHIMISHA JUMA LA ELIMU YA WATU WAZIMA NA ELIMU NJE YA MFUMO RASMI

    September 05, 2025
  • ELIMU IENDELEE KUTOLEWA KWA WANANCHI KULA VYAKULA VYENYE LISHE ILI KUPUNGUZA UTAPIAMLO

    September 05, 2025
  • Angalia zote

Video

Mvamizi wa eneo la soko.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Istagram page
  • Dira na Dhamira
  • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Mpango Mkakati
  • Mpango wa Uwekezaji Sekta ya Samaki
  • Muundo wa Taasisi
  • OPRAS - Form
  • Baraza la Madiwani

Viunganishi Muambata

  • Matokeo ya Darasa la Saba 2023 Bundadc
  • Matokeo ya darasa la saba
  • Matokeo ya darasa la saba
  • PO-RALG
  • PO-PSM
  • Matokeo ya Kidato cha Nne 2019

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Kibara Stoo.

    Anuani ya Posta: 126, Bunda

    Simu: 0282621055

    Hamishika:

    Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda