Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mh. Aswege Enock Kaminyoge siku ya tarehe 2/6/2025 alifanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya Maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda inayoendelea kutekelezwa.
Mh. Kaminyoge aliongozana na kamati ya usalama ya Wilaya, Katibu Tawala wa Wilaya, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, pamoja na baadhi ya wataalamu wa Halmashauri.
Katika ziara hiyo Mkuu wa Wilaya alitembelea ukamilishaji wa shule ya Sekondari Mayolo, Chanzo cha maji kilichopo Bulamba ambacho kinasambaza maji yake hadi Kijiji cha jirani cha Kabainja, pia, alitembelea na kukagua ukamilishaji wa daraja lililopo Mariwanda- Steven Wasira, nyumba za walimu ( 2 in 1) katika shule ya msingi Sabasita, na ukamilishaji wa Madarasa matatu na matundu sita ya vyoo katika shule ya msingi Igundu.
Mh. Kaminyoge aliridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa miradi hiyo, na alimuagiza Mkurugenzi Mtendaji kuhakikisha anarekebisha kasoro ndogo ndogo zilizoonekana katika baadhi ya miradi, wakishirikiana na Mhandisi wa Halmashauri, kwani kwenye baadhi ya majengo yalionekana kuwa na changamoto chache ambapo alitoa siku 14 kuhakikisha changamoto hizo zinarekebishwa na kuikabidhi miradi hiyo.
Aidha, katika ziara hiyo, Mh. Mkuu wa Wilaya alikamata dhana haramu za uvuvi wa samaki kwa jina maarufu kokoro katika ufukwe wa Bulamba, ambapo walikuwa wakitumia kuvua samaki kwa kutumia nyavu hizo.
Mh. Kaminyoge alikemea uvuvi haramu unaoendelea katika ziwa Viktoria kwani ndio umekuwa Chanzo cha kukosekana kwa samaki kutokana na watu kuvua samaki ambao Bado hawajakomaa na kuwa tayari kwa kitoweo.
Mkuu wa Wilaya aliagiza kukamatwa kwa nyavu hizo na kuhakikisha hatua Kali za kisheria zinachukuliwa ili kukomesha uvuvi haramu katika Ziwa Viktoria.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika:
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda