Kamati ya siasa ya Wilaya ya Bunda ikiongozwa na Mwenyekiti wa Chama (CCM) Ndugu Mayaya A. Magesse imeupongeza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda kwa usimamizi wao mzuri katika mradi wa ujenzi wa shule ya sekondari ya wasichana Mara, iliyopo katika kijiji cha Bulamba Kata ya Butimba.
Pongezi hizo zilitolewa na kamati ya siasa ya Wilaya ya Bunda walipofanya ziara siku ya tarehe 16/5/2024 ya kutembelea na kukagua maendeleo ya mradi huo.
Wajumbe wa kamati ya siasa walitembelea na kukagua jengo moja baada ya lingine, ikiwemo na miundombinu yote iliyopo katika shule hiyo ya wasichana Mara ambapo walimpongeza Mkuu wa Wilaya ya Bunda, pamoja na uongozi mzima wa Halmashauri kwa usimamizi wao mzuri.
Katika ziara hiyo, wajumbe walishauri ulinzi katika eneo hilo uongezwe na kuhakikisha wanajenga uzio mapema ili kuzuia masuala ya wizi na kulinda mali zote zilizopo eneo la mradi.
Kamati pia, walishauri Halmashauri ihakikishe wanachimba kisima cha kuhifadhi maji, na kuhakikisha wananunua matanki kwa ajili ya kuvunia maji ya mvua badala ya kutegemea maji ya bomba pekee, pia, walishauri zifungwe solar katika shule hiyo ambapo zitasaidia kuimarisha ulinzi na usalama wa eneo hilo pale umeme wa TANESCO utakapokuwa umekatika.
Ndugu Magesse alimshukuru Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kukubali kujenga mradi huu mahali hapa na alisisitiza suala la kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha changamoto zote zilizobainishwa na wajumbe wa kamati zinarekebishwa na aliwataka wananchi kuwa walinzi wa shule pamoja na miundombinu yote iliyopo katika eneo hilo la mradi, kwani wao ndio wanufaika wakuu katika mradi huo.
“Endeleeni kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na msikate tamaa katika kusimamia miradi mingine ya maendeleo na mfanyekazi kwa bidii.” Alisema Ndugu Magesse.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mh. Dkt. Vicent Anney alisema ulinzi wa eneo hilo kwa sasa umeimarishwa zaidi tofauti na hapo awali, na alimuhakikishia Mwenyekiti wa kamati kuwa kazi zinafanyika vizuri na Halmashauri inasimamia vizuri mradi huo kwa kuhakikisha unajengwa kwa viwango sahihi na kukamilika kwa wakati.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0754335739
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda