Halmashauri ya Wilaya ya Bunda imeadhimisha siku ya wazee duniani ambapo maadhimisho hayo yamefanyika katika Kata ya Hunyari siku ya tarehe 1/10/2024, na mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, Ndugu Noel Shamazugu.
Ndugu Shamazugu aliwashukuru wazee wote waliojitekeza katika madhimisho hayo ambapo alisema lengo kuu la kuadhimisha siku hii ni kwa ajili ya kuongeza uelewa katika jamii kuhusu masuala mbalimbali ya wazee ikiwa ni Pamoja na kutafakari fursa na changamito zinazowakabili wazee na kuona ni namna gani wataweza kuzitatua changamoto hizo.
“Katika kutimiza adhima ya wazee kwa kuwafanya waishi Maisha mazuri na kuwapa huduma nzuri, serikali ipo katika hatua za mwisho za kuboresha sera za wazee kwa kuona ni namna gani watazitatua changamoto zao.” Alisema Ndugu Shamazugu.
Alisema, mikakati ya serikali ni kuendelea kufanya utambuzi wa wazee wote waliopo ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, ambapo kwa mwaka huu 2024 jumla ya wazee 6302 tayari wameshatambuliwa hivyo, watapatiwa vitambulisho vya msamaha wa matibabu. Serikali imeendelea kuwaunganisha wazee na mfuko wa TASAF ili waweze kujiendesha maisha yao wenyewe pasipo kuwa tegemezi katika jamii.
“Tunaamini kupitia mfuko huu wa TASAF ambao huwa unatolewa kwa walengwa kwa kipindi cha miaka mitano mzee utakuwa umeshajipanga vizuri kwa kuanzisha mradi hata wa ufugaji mbuzi ambao watakusaidia katika kuendesha maisha, miaka mitano inapoisha huwa wanawaondoa walengwa wa awamu ya kwanza na kuwekwa wengine. Hivyo mzee unapopata fursa hii ya kuingia kwenye mfuko wa TASAF unatakiwa zile fedha unazozipata uanze kufikiria mradi wa kufanya na sio kula tu maana miaka mitano inapoisha serikali inaamini utakuwa umesogea kwa sehemu Fulani.” Alisema Kaimu Mkurugenzi.
Halmashauri tunaendelea kupokea na kufanyia kazi malalamiko na changamoto mnazokabiliana nazo kupitia serikali za vijiji na vitongoji kwa kuhakikisha tunaboresha na kutatua changamoto hizo, tunaendelea kuboresha na kuanzisha madirisha ya wazee katika vituo vya Afya na hospitali zetu, ili mzee unapoenda kupata huduma uhudumiwe kwa haraka na sio kupanga foleni muda mrefu kusubiria.
Katika kuadhimisha siku ya Wazee duniani huduma mbalimbali ziliweza kutolewa ikiwemo ugawaji wa dawa bure, upimaji wa Afya, ugawaji wa vitambulisho vya msamaha vya matibabu na upimaji wa hali ya Lishe.
Naye Afisa Ustawi ustawi wa jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, Bi. Fausta Gabriel alitoa elimu mbalimbali kwa wazee kuhusiana na ukatili wa wazee, haki za wazee, elimu ya bima ya Afya ya iCHF na elimu kuhusu haki za wazee kwa mujibu wa sera yam waka 2003.
Katika maadhimisho hayo Halmashauri iliweza kuzindua Program Jumuishi ya Taifa ya Malezi Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto kwa ngazi ya Kata.
Kibara Stoo.
Anuani ya Posta: 126, Bunda
Simu: 0282621055
Hamishika: 0754335739
Barua Pepe: ded@bundadc.go.tz
Haki Miliki@ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda